Nyota wa Arsenal, Theo Walcott ametengewa dau la Pauni 30 na klabu ya Everton ikiwa ni mipango ya kocha Ronald Koeman kukisuka kikosi chake msimu huu mpya.
Walcott mwenye miaka 28 alikuwa kwenye kiwango ha juu misimu kadhaa iliyopita, ikilingwanisha na sasa.Mchezaji huyo ameonyeshwa mlango wa kutokea iwapo klabu itafikia dau lililowekwa.
Mshambuliaji huyo anapewa nafasi kubwa kutua Everton kutokana na klabu hiyo kuwa na mkakati wa kumariha safu yake ya ushambuliaji.
Koeman pia anataka kumchukua mshambuliaji mwingine wa Arsenal, Olivier Giroud ambaye amemtengea Pauni 20 milioni.