F Flora Mbasha awafungukia wanaomchafua mtandaoni | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Flora Mbasha awafungukia wanaomchafua mtandaoni

Msanii wa nyimbo za Injili Tanzania, Flora Mbasha

Msanii wa nyimbo za Injili Tanzania, Flora Mbasha amevunja ukimya na kutoa onyo kwa baadhi ya watu wanaomchafua kupitia mitandao ya kijamii hususan Instagram.

Flora ambaye kwa sasa ameolewa na mwanaume mwingine baada ya kutengana na mume wake wa awali ambaye pia ni mzazi mwenziye, Emmanuel Mbasha, amelazimika kutoa onyo hilo baada ya kusambaa kwa taarifa mitandaoni akinukuliwa kwamba mzazi mwenziye huyo hakuwahi kumridhisha kimapenzi kwa kipindi chote walichokuwa kwenye ndoa.

Flora amekana taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika hivi:

“Hizi habari ni za uongo, sijafanya mahojiano na redio yoyote na kuzungumza maneno hayo kama ilivyosambaa mitandaoni. Naomba mzipuuze taarifa hizo maana ni mpuuzi mmoja tu ameamua kuonesha upuuzi wake ili apate followers kwenye ukurasa wake.

“Niseme tu kwamba hivi sasa sitakaa kimya tena, huyo aliyezoea kunizushia stori za uongo asifikiri siijui sheria, ajipange vizuri maana mahakama ipo na sheria ipo, narudia tena kusema habari hii iliyosambaa mitandaoni ni ya uongo sijazungumza mimi maneno hayo.”