Uamuzi huo unatokana na Pingamizi la Dhamana liliwasilishwa Mahakamani hapo Juzi na Jopo la Mawakikli wa Serikali.
Mawakili wa Serikali waliibua Mahakamani hapo hoja ya kuzuiliwa kwa dhamana ya Lissu kutokana na kushtakiwa na makosa ya uchochezi zaidi ya nne Mahakamani.
Jopo la Mawakili wa Utetezi lipinga hoja hizo kwa kudai kwamba Dhamana ni haki ya Mshtakiwa na kwamba Mashtaka ya Lissu yanadhaminika.