F Machifu wa wasukuma wafunguka ishu ya Wanafunzi kubeba mimba | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Machifu wa wasukuma wafunguka ishu ya Wanafunzi kubeba mimba

Machifu na watemi wa kabila la wasukuma wa mikoa ya kanda ya ziwa kwa pamoja wameunga mkono kauli ya Mh.Rais John Pombe Magufuli ya kutosomesha wanafunzi wakike watakaopata mimba huku wakiahidi kusimamia mila na desturi zenye maadili mema kwa jamii na kupiga vita mila na desturi potofu zinazotajwa kusababisha uwepo wa mimba na ndoa za utotoni pamoja na mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi.

Akitoa kauli hiyo kwa niaba ya machifu na watemi wa kabila la wasukuma katika Sanjo ya Busiya wilayani kishapu chifu wa ukoo wa Busya Eduward Makwaia amesema kwa kauli moja wanaunga mkono utendaji wa Mh.Rais John Pombe Magufuli huku askofu wa jimbo katoliki la Shinyanga Mhasham baba askofu Liberatus Sangu akiwataka watanzania kuenzi mila na desturi zenye maadili mema na kuacha mila potofu ambazo zinatajwa kusababisha vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto wakike.

Naye mwenyekiti wa chama cha watu wenye ualibino Tanzania Bw.Nemes Temba amewashukuru machifu wa kabila la wasukuma kwa kuweza kuwakutanisha watu na kutoa mafundisho yenye maadhili kwa njia ya ngoma na michezo mbalimbali iliyolenga kutoa ujumbeu muhimu juu ya athari za matendo ya kikatili katka jami.

Meneja mauzo wa kampuni ya simu za mikononi ya tigo mkoani Shonyanga Bi.Idda Johnson Kapola amesema kampuni ya tigo imejikita moja kwa moja katika kupiga vita mila na desturi potofu zinazomnyima haki mtoto wakike huku meneja wa crdb baank tawi la shinyanga bw.saidi pamui akitoa zawadi kwa washindi watatu wa utunzaji wa mazingira wilayani kishapu na kuahidi kusimamia zoezi la utunzaji wa mazingira mkoani humo.