F Maua Sama afunguka kuteswa na mapenzi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Maua Sama afunguka kuteswa na mapenzi

STAA wa Ngoma ya Mahaba Niue, Maua Sama amefunguka siri yake ya kuwa mtaalamu wa kuimba nyimbo zinazohusu mapenzi kwamba ni kutokana na kuteswa na kupondwapondwa kama nyanya na uhusiano wa kimapenzi hivyo kumpa somo.

Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Maua Sama alisema kuwa, amekuwa mwimbaji mzuri wa nyimbo za kimapenzi kwa sababu alipata somo kubwa kwenye maisha aliyoishi na mpenzi wake aliyemfanya kuiona dunia chungu.

“Mapenzi yalinipondaponda kama nyanya na kunifanya dunia niione chungu. Pamoja na maumivu yote, lakini nimekuwa ni mtu niliyejifunza mambo mengi kwenye mapenzi ndiyo maana hata nikiandika ngoma ya mapenzi, lazima itapokelewa vizuri na watu kibao,” alisema Maua.