F Mimba ya Kajala ilivyo yeyuka | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mimba ya Kajala ilivyo yeyuka

MIEZI kadhaa iliyopita, mkali wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ aliripotiwa kunasa ujauzito ambao uligeuka matangazo kwenye baadhi ya akaunti za Instagram, lakini hivi karibuni alionekana akiwa hana kitumbo wala kitambi, jambo lililomlazimu mwanahabari wetu kumhoji kulikoni kuyeyuka kwa mimba na kueleza ilivyotoka.

Katika majibu yake, Kajala alidai kuwa, kibendi chake kilichoropoka baada ya kupata uvimbe mkubwa tumboni.

Ishu ya Kajala kuwa mama kijacho ilienea kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo aliorodheshwa kwenye listi ya mastaa wenye ujauzito Bongo.

Habari za ujauzito wa Kajala ziliambatanishwa na picha zilizomuonesha akiwa mnene, jambo alilolikwepa kwa kuwa hapendi kuongezeka mwili ndicho kigezo kilichotumika kujulikana mapema kuwa ‘ameshiba’. Baada ya ishu hiyo kusambaa, wengi walikuwa wakiandika stori za kutaka kujua mwanaume aliyempachika Kajala kibendi huku mwenyewe akiweka ngumu kumuanika.

Hata hivyo, kadiri siku zilivyosonga, joto la mimba ya Kajala lilikuwa likishuka kidogokidogo hadi kufi kia nyuzi sifuri baada ya kuonekana akijiachia kwenye viota vya burudani akiwa amevaa nguo za kumbana, kuashiria kuwa hakuwa tena na ujauzito kama watu walivyokuwa wakisema.

Katika mahojiano na gazeti hili nyumbani kwake, TRAMwenge jijini Dar, juu ya sintofahamu ya jambo hilo, Kajala alikiri kupata ujauzito, lakini haukuwa riziki kwani alikuwa na uvimbe mkubwa tumboni uliosababisha ujauzito huo kuchoropoka. “Unajua huwezi kumuelezea kila mtu nini kimekupata kwa sababu mambo mengine ni ya kibinafsi zaidi, lakini ukweli ni kwamba uvimbe ulisababisha mimba yangu kutoka na hiyo nilijua baada ya kwenda Hospitali ya Aga Khan (Dar) kufanya vipimo,” alisema Kajala.

Staa huyo aliongeza kuwa, pamoja na uvimbe kuwa sababu kubwa, pia mazoezi nayo yalichangia ambapo baada ya kukumbwa na tatizo hilo daktari alimshauri kupumzika mazoezi kwa muda.

“Pamoja na kwamba uvimbe ulikuwa ndiyo sababu kubwa, lakini daktari alinishauri hata mazoezi nipumzike kwa muda kwanza ndiyo nitaendelea nafi kiri na kunenepa ndiyo kukaongezeka,” alisema Kajala ambaye bado aliendelea kufanya siri juu ya mwanaume aliyesababisha ujauzito huo. Kajala ni mama wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Paula Paul aliyezaa na Bosi wa Bongo Records, Paul Mathyasse ‘P-Funk Majani’