Katika salamu hizo, Rais Magufuli ameelezea kushtushwa na kusikitishwa na kifo hicho, na kusema yeye na familia yake wanaungana na familia ya Dkt. Mwakyembe katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
“Nakupa pole sana Dkt. Mwakyembe kwa kuondokewa na mkeo mpendwa Bi. Linah, natambua hisia za maumivu ulizonazo wewe na familia nzima, nyote nawaombea Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Namuombea Marehemu Linah George Mwakyembe apumzishwe mahali pema peponi, Amina”, amesema Mhe. Rais Magufuli.