F Serikali imelifungua Gereza la kitengule | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Serikali imelifungua Gereza la kitengule

Serikali imelifungua tena Gereza la Kitengule lililoko wilayani Karagwe lililofungwa septemba 18, mwaka jana baada ya kubolewa na tetemeko la ardhi lilitokea mkoani Kagera na kusababisha madhara makubwa ambayo ni pamoja na vifo vya watu 17 hali iliyoilazimu wafungwa 241 waliokuwa ndani ya Gereza hilo kuhamishiwa kwa muda katika gereza la Mwisa ambalo ni maalumu kwa ajili ya kuwahifadhi wakimbizi wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali.

Gereza hilo ambalo lilibomolewa vibaya na tetemeko hilo kiasi cha baadhi ya kuta kuanguka kabisa limefunguliwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Lameck Nchemba baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa, akizungumza amesema serikali ililazimika kulifunga gereza hilo na kuwahamisha wafungwa kwa kuwa lilikuwa linahatarisha usalama wa maisha yao. 

Kwa upande wake, kamishina Jenerali wa jeshi la Magereza Dkt. Juma Malewa ameishukuru kamati iliyokuwa ikiratibu maafa ya tetemeko na uongozi wa mkoa wa Kagera kwa kutoa fedha za vifaa vya kukarabati gereza hilo, naye mkuu wa Magereza katika mkoa wa Kagera Jeremiah Nkondo amesema uamuzi uliochukuliwa na serikali ya kulifunga gereza hilo ulikuwa wa busara kwa kuwa baadhi ya kuta za gereza hilo zilikuwa zimewekewa miti, huku mkuu wa gereza la Kitengule, Robert Masali akisema kuwa gereza baada ya kukarabatiwa litakuwa na uwezo wa kuwahifadhi wafungwa 278.