Shilole aja na kigoli

MWANAMUZIKI mwenye jina hapa Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameibuka na kusema kuwa yupo mbioni kutoa Ngoma ya Kigoli mwishoni mwa mwezi huu ambao utakuwa na ma­hadhi ya Afropop.

Shilole ambaye amewahi kutamba na nyimbo zake kadhaa zikiwemo Say My Name, Hatutoi Kiki, Malele na nyinginezo kibao, amese­ma ngoma hiyo ina ujumbe mzuri kwa jamii hivyo mashabiki wake wajiandae kuipokea.

“Natarajia kutoa wimbo mpya mwishoni mwa mwe­zi huu, nimeimba mahadhi ya Afropop naamini uki­toka tu na watu wakiusikia utakuwa funzo kwa jamii kutokana na ujumbe uli­omo humo,” alisema Shilole.