Staa wa Bongo, Agnes Gerald Wire maarufu kwa jina la Masogange akiwa mahakamani.
HATIMAYE kesi inayomkabili mwanadada Agnes Gerald Wire maarufu kwa jina la Masogange akidaiwa kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya imechukua sura mpya baada ya kusomwa kwa mara nyingine katika mahakama ya Kisutu jijini Dar.
Katika kesi hiyo ambayo imeahirishwa huku ikitarajiwa kutajwa Agosti 28 mwaka huu, ilielezwa mahakamani hapo kwamba dada huyo alifanyikwa vipimo vya kemikali kupitipia mkojo wake kwa kutumia kifaa maalum na kugundulika kuwa chembechembe za madawa ya kulevya aina ya heroine.