Uchunguzi uliofanywa kwenye mwili wa aliyekuwa mkuu wa idara ya Tehama ya tume ya uchaguzi ya Kenya Bw Chris Msando, umeonyesha kuwa aliteswa na kuuawa.
Kwa mujibu wa mwanapatholojia mkuu wa serikali Dk Johansen Oduor na daktari wa familia Dk Bessie Byakika, mwili wa Bw Msando umeonesha kuwa wauaji walitumia mikono kumnyonga na pia walimpiga na kitu chenye ncha kali na kumsababishia jeraha.
Matokeo ya uchunguzi wa kipatholojia umekuwa ni msingi wa uchunguzi kufuatia kifo chake, na tayari watu watatu wametiwa mbaroni kuhusiana na kifo cha Bw Msando, lakini bado haijulikani walihusika vipi na kifo chake.
Mwili wa Bw Msando pamoja na wa msichana mwanafunzi mwenye umri wa miaka 21 uliokotwa jumamosi kwenye msitu wa viunga vya Nairobi.