Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi ni Boniface Wambura.
KAIMU Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Kidao amesema kuwa ameagizwa na rais wa Shrikisho hilo, Wallace Karia kumwandikia barua Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi ili kuwaadhibu viongozi wa Bodi ya Ligi waliohusika na kupanga ratiba.
Kumekuwa na malalamiko kutokana na Bodi hiyo kupanga ratiba ya ligi ambapo walishindwa kuzingatia kuwa kuna michezo ya kimataifa ambayo itahusisha timu za taifa jambo ambalo limesababisha baada tu ya mchezo mmoja tu, ligi hiyo ikapanguliwa tena.
“Nimeagizwa na rais nimwandikie barua mtendaji mkuu wa bodi ya ligi ili aweze kuwachukulia hatua viongozi wa bodi hiyo waliohusika na kupanga ratiba hii pamoja na kwamba walikuwa na kalenda lakini bado wamekosea,” alisema Kidao.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi ni Boniface Wambura ambaye sasa atakuwa na jukumu la kuchukua hatua kwa wasaidizi wake.