F Watuhumiwa wa kula nyama za watu waendelea kushikiliwa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Watuhumiwa wa kula nyama za watu waendelea kushikiliwa

Wanaume wanne ambao wanatuhumiwa kuwala watu nchini Afrika Kusini wametupilia mbali ombi lao la kutaka kuachiliwa kwa dhamana.

Wanne hao walikuwa wamefika kortini kwa kikao cha kuomba dhamana lakini hata kabla ya ombi lao kusikilizwa katika mahakama ya Estcourt.

Kesi yao itatajwa tena mwishoni mwa mwezi ujao.

Mwandishi wa BBC Nomsa Maseko aliyekuwepo mahakamani anasema mmoja wao alikuwa anatokwa na machozi.

Nje ya ukumbi wa mahakama, makundi ya watu waliandamana kupinga kuachiliwa huru kwa washukiwa hao kwa dhamana.

Miongoni mwa walioshtakiwa ni mganga wa kitamaduni ambaye anatuhumiwa kuwafanya wateja wake wale nyama ya binadamu kwa ahadi kwamba ingewasaidia kutajirika na kufanikiwa maishani.

Walikamatwa baada ya mmoja wao kudaiwa kufika katika kituo cha polisi na kuambia maafisa wa polisi kwamba alikuwa "amechoka" kula nyama ya binadamu.

Alipohojiwa zaidi, mwanamume huyo alichomoa mguu na mkono wa binadamu.

Polisi kisha waliandamana na mwanamume huyo hadi kwenye nyumba moja

KwaZulu-Natal ambako viungo zaidi vya binadamu vilipatikana.

Baadhi ya walioandamana nje ya mahakama leo walikuwa na mabango na walikuwa wakiimba kwa Kizulu: "Tunataka kuwaona wauaji."

Wengine walikuwa wakiimba: "Sisi sio Hungry Lion, na wala sio Nando's. Sisi ni binadamu na hatufai kuliwa."

Hungry Lion na Nando's ni maduka mawili maarufu kwa uuzaji wa chakula nchini humo.