F Wolper: Hii hali inatishia taifa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wolper: Hii hali inatishia taifa


Msanii wa filamu bongo, Jacqueline Wolper.

Msanii wa filamu bongo, Jacqueline Wolper aumizwa baada ya kuona idadi kubwa ya watu waliojitokeza kufanya usaili wa TRA jana na kusema anawaonea huruma yatima ambao hawana mtu wa kuwapigania ili kuweze kupata kazi hizo.

Wolper amebainisha hayo baada ya picha iliyokuwa ikionyesha umati wa vijana waliojitokeza kwa wingi kufanya usaili  wa TRA kwa awamu ya kwanza ambao umefanyika jana na kuendelea leo ambao umeandaliwa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

"Nikiangalia picha kama hizi naumiaga sana na nilivyo na machozi ya karibu basi nalia kabisa. Yaani naona hata wadogo zangu ni miongoni mwa hawa wanaopigania nafasi ya kupewa kazi na ukizingatia nimesomesha kwa tabu sana tena nilikuwa sina hata biashara huku nikisaidiana na wazazi wangu. Roho inauma pale ambapo mdogo wako anakwambia Dada nimepata kazi ya kujishikiza kwa wiki tatu nitalipwa laki na nusu kule Mkoani Mbeya kijijini tena hapo ni uliyemfikiria akipata 'degree' yake atakuja japo kuinua familia ama ajitegemee mwenyewe lakini siyo hivyo", aliandika Wolper.

Pamoja na hayo, Wolper aliendelea kwa kusema "mimi najiuliza unaposema ipo siku sijui hiyo siku ni ipi. Haya wote hao waliojitokeza huku wanaohitajika ni wachache yaani kwa uwiano ni kama mtu mmoja achaguliwe kati ya watu 140 kwa sababu ni watu 56,000 kwa nafasi 400 kama 'data' ziko sahihi, Mungu wangu bora hata mdogo wangu ataomba hela ya vocha na kula na kulala atapata.

Lakini vipi waliyosomeshwa na wazazi wa kambo au kwa msaada", alihoji Wolper.

Jacqueline Wolper siyo mtu wa kwanza kuonyesha hisia zake juu ya tukio lililotokea siku ya jana katika usaili huo kwa maana kila aliyeweza kuona picha hiyo hakuweza kujizuia kutoa dukuduku lake la moyoni.


Hii ndiyo picha ambayo imegusa hisia za watu wengi