F Bomoa bomoa: Wananchi wa Jangwani Dsm walivyopambana na Polisi leo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Bomoa bomoa: Wananchi wa Jangwani Dsm walivyopambana na Polisi leo

Wakazi wa Jangwani jijini Dar es Salaam, leo wamepambana na polisi na kusababisha vurugu katika barabara ya Morogoro.

Wananchi hao walikuwa wakizuia tingatinga la bomoa bomoa lisibomoe nyumba zao zilizoko bondeni kwa kuwarushia mawe hatua iliyowalazimu kutoa taarifa  polisi ambao walikuja baada ya muda mfupi na kuwatawanya kwa kufyatua risasi na mabomu ya machozi huku wananchi hao akiwarushia mawe polisi hao.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema wananchi hao wamedhibitiwa na zoezi la ubomoaji linaendelea.

Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa, hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo.