F Dar es salaam kutangazwa nchini China | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Dar es salaam kutangazwa nchini China


MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Sa laam Isaya Mwita leo amekutana na kufanya mazungunzo na Meya wa Jiji la Xin'an Nchni China Zhu Huan ofisini kwake Karimjeee.

Katika mazungumzo hayo , Meya Mwita na mgeni wake wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kukuza na kutangaza utalii wa ndani na nje ya Dar es Salaam.

Aidha Meya Mwita amesema jiji la Dar es Salaam lina kila aina ya vivutio vya utalii wa ndani na nje ambavyo vinaweza kuwavutia wageni mbalimbali kutoka nje ya Nchi kufika jijini hapa na kutalii badala ya kwenda  Zanzibar , Kilimanjaro na maeneo mengine.
Ameongeza kuwa anaamini kuwa mazungumzo hayo na mgeni wake yataleta tija na kwamba jiji la Dar es Salaam litapata watalii kutoka sehemu mbalimbali na hivyo kuliwezesha jiji kupata mapato makubwa kupitia vivutio vilivyopo.

“ Tunania ya kulitagaza jiji letu kwenye sekta ya utalii, kutokana na rasilimali za vivutio vilivyopo, ukienda kwenye maeneo mengi ndani ya jiji letu utaona kuwa tunavyo vivutio vyakutosha kabisa ambavyo vikitangazwa kila mmoja atapenda kutalii katika jiji hili” amesema Meya Mwita.

“ Yapo maeneo mengi ambayo watanzania hawayajui, lakini kupitia mpango huu ambao nimekuja nao hivi sasa ninaimani kwamba watu ambao walikuwa wanafika kwenye jiji letu na kupanda ndege kwenda Zanziba ama Arusha na maeneo mengine, sasa watafanya utalii hapa kwetu” amesisitiza.
Meya Mwita ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa , hivi karibuni jiji la Dar es Salaam linaratajia kupokea magari ya utalii ambayo yamenunuliwa kupitia fedha za jiji, ambapo baada ya kufika yatazinduliwa na hivyo kuanza kutangaza utalii wa ndani.

Kwaupande wake Meya wa jiji la Xin’an Zhu Huan amempongeza Meya Mwita kutokana na uendeshaji wake wa jiji, ambapo amesema jiji la Dar es Salaam limepata Meya bora ambaye anaamini kwamba ataleta mabadiliko makubwa ndani jiji hili.

Mbali na pongezi hizo, pia ameahidi kushirikiana nae katika sekta mbalimbali ikiwemo kutangaza utalii wa jijini hapa ili uweze kutambulika katika maeneo mengine Nchini China.