F Kupigwa risasi Lissu kumeitia doa nchi: Askofu Shoo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kupigwa risasi Lissu kumeitia doa nchi: Askofu Shoo


Aliyekua Askofu wa Kanisa la TAG Mkoa wa Kilimanjaro, Gloroius Shoo amesema kitendo cha kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kumeitia doa nchi.

Alisema nchi itapoteza sifa ambayo iliijivunia ya kuitwa kisima

cha amani kwa miaka mingi duniani kutokana na vitendo viovu

vinavyozidi kujitokeza vya umwagikaji wa damu pamoja na utekaji unaoendelea kwa sasa.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake leo Jumamosi Askofu Shoo amesema sifa ya amani imesababisha watu mashuhuri kuja nchini pamoja na ujio wa wawekezaji wengi bila kuhofia usalama wao kutokana na amani iliyokuwepo.

Shoo amesema kuwa watu waliofanya unyama huo walikua na kiburi kikubwa kutokana na uthubutu wao wa kufanya mchana katikati ya makao makuu ya nchi.

“Ninakemea vikali umwagikaji wa damu kwa viongozi wetu, huu ni udhalilishaji mkubwa na haukubaliki kwa taifa hili la

Tanzania, ninaomba Serikali kwa nguvu zote ihakikishe inawatia mikononi wote wanaohatarisha usalama wa nchi yetu,” alisema Askofu Shoo.

“Uthubutu huo lazima uingiliwe kati na Serikali la

sivyo itatuondolea  sifa ya nchi yetu na huu ni udhalilishaji

mkubwa.”