Gabriel Jesus akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Manchester City dakika za 45 na ushei na 53 katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo mchana Uwanja wa Etihad. Leroy Sane alitokea benchi kuchukua nafasi ya Jesus dakika ya 57 naye akafunga mabao mawili dakika za 77 na 90 na ushei, wakati bao la kwanza leo lilifungwa na Sergio Aguero dakika ya 24.