F Mbaraka Yusuph afunguka, Kila mechi kwetu ni Fainali | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mbaraka Yusuph afunguka, Kila mechi kwetu ni Fainali

Mshambuliaji tegemeo wa Azam FC, Mbaraka Yussuf

Mshambuliaji tegemeo wa Azam FC, Mbaraka Yussuf amesema kila mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kwao ni kama fainali.

Mbaraka Yussuf amesema wanajua ya kuwa kila mchezo wanaocheza unakuwa mgumu kutokana na timu pinzani kuwakamia, lakini amedai malengo yao ni kushinda kila mtanange.

“Kwanza namshukuru Mungu kucheza mechi hizi salama pia namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kufunga pia napenda sana kujitahidi kadiri ya uwezo wangu kila mechi niwe naweza kufunga ili niweze kuweka rekodi nzuri katika msimu huu na nawaahidi mashabiki kuwa mfungaji bora” amesema Mbaraka Yussuf

Akizungumzia kuhusu mchezo ujao dhidi ya Singida United, Mbaraka amesema:

“Kwa kweli mechi yoyote ile Azam ikikutana na timu yoyote mechi inakuwa ngumu kwa vile watu wanakuwa wanakamia sana, kauli mbiu yetu kila mechi sisi kwetu ni fainali na tunapambana ili tuweze kufunga. ” amesema.