F Waziri mkuu wa Australia akubali ndoa ya jinsia moja | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Waziri mkuu wa Australia akubali ndoa ya jinsia moja


Viongozi wa siasa nchini Australia akiwemo waziri mkuu Malcolm Turnbull, wameunga mkono kampeni inayopigia debe ndoa ya jinsia moja.

Zaidi ya watu 20,000 walikusanyika mjini Sydney kwenye kampeni kabla ya kura ya maoni isiyo rasmi ya kubadilishwa sheria za ndoa nchini Australia.

Bwana Turnbull alijitokeza kwa ghafla na kutoa hotuba wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo huko New South Wales.

Kiongozi wa upinzani Bill Shorten kisha akahutubia umati kwenye mkutano mkuu.

Kura hiyo ya kubadilisha sheria ya ndoa inapigwa kwa njia ya posta kuanzia Septemba 12 na matokeo yakitarajiwa mwezi Novemba.

Kura hiyo haitakuwa na uwezo wa kuhalalisha ndoa ya jinsia moja, lakini itachangia kura kupigwa bungeni ikiwa asilimia kubwa na watu nchini Australia wataunga mkono mabadiliko hayo.

Awali waziri mkuu alisema kuwa yeye binafsi atapiga kura kuunga mkono ndoa ya jinsia moja lakini hajafanya kampeni hadharani kabla ya hotuba ya kungashaza leo Jumapili.

Bwana Turnbull alisema kuwa nchi zingine 23 tayari zimehalalisha ndoo ya jinsia moja.