F Kichuya awapiga mkwara Yanga, asema ni wepesi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kichuya awapiga mkwara Yanga, asema ni wepesi

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya Yanga, kwamba wapinzani wao hao ni wepesi na watawafunga leo.

Kichuya amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanjani bila ya hofu kwani ana uhakika wa ushindi kutokana na maandalizi yao chini ya Kocha Joseph Omog.

Kichuya alisema, katika mechi hiyo kikubwa wao kama wachezaji wamepania kupata ushindi ili waendelee kubaki kileleni katika msimamo ya ligi.

 “Tunajua kabisa mashabiki wa Simba kitu gani wanakitaka katika mechi hii dhidi ya Yanga, hivyo niwatoe hofu kwa kuwaambia kuwa waje kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kutushangilia.

“Watarajie matokeo mazuri ya ushindi na soka safi kutoka kwetu kutokana na maandalizi tuliyoyafanya kambini Zanzibar, sisi wachezaji tunataka pointi tatu ili tubaki kileleni,” alisema Kichuya.

Katika mchezo wa ligi kuu msimu uliopita wa Februari 25, mwaka huu ambao Simba ilishinda mabao 2-1, Kichuya alifunga bao moja kati ya mawili ya timu yake.

SOURCE: CHAMPIONI