Naibu waziri atoa agizo kwa wakurugenzi wote nchini



Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo na makazi Angelina Mabula amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri kuweka utaratibu Wa kupanga miji kama sehemu ya yao kuliko kukurupuka na mashinikizo ya viongozi au makundi ya watu wenye uhitaji aridhi.


Ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati maadhimisho ya siku ya makazi duniani katika viwanja karimjee alipokua anazungumza wa wadau.

"Halmashauri ndio zenye jukumu kubwa kupanga miji na hawawezi kulikwepa hilo lakini cha ajabu halmashauri nyingi zimekua zikipima miji kwa mashinikizo ya makundi ya watu hali inayofanya kuibuka kwa miji kiholela katika makazi yetu". amesema Mabula.

Aliongeza kwa kusema kuwa siku ya makaziitakumbusha umuhimu wa kuwa na makazi bora yanayoendana na miundombinu ya huduma za kijamii.

Aidha Naibu waziri Mabura ameweka wazi kuwa kwa sasa wizara yake imeweza kurasimisha nyumba zaidi ya 2000 katika eneo la Kimara na Mbezi lakini haijamaanisha kuwa zoezi hilo litaweza kuendelea nchi nzima katika maeneo ambayo yamejengwa kiholela.

Serikali itaendelea kusimamia mpango kabambe yaani (master plan) wa miji yote ikiwemo baadhi ya mikoa ikiwemo Mtwara, na Mwanza hivyo hawatakuwa na msamaha new wote watakaokwenda kinyume na utaratibu Wa mpango huo.