F Ofisi za Manji zafungwa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Ofisi za Manji zafungwa

Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji ameendelea kuingia matatani baada ya Kampuni ya Udalali ya Yono kuzifunga ofisi zake zilizopo Barabara ya Pugu.

Yono wamezifunga ofisi na maghala ya Manji ambaye alikuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga akituhumiwa kudaiwa kodi ya zaidi ya Sh300 milioni na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Yono, Scholastika Kevela amesema, ‘’ni kweli tumezifunga ofisi za Manji zilizopo eneo la Pugu, anadaiwa fedha nyingi za kodi na TRA.”

Alipoulizwa kipi kitafuata baada ya kuzifunga, Kevela amesema, ‘’sisi utaratibu wetu ni kwamba tukizifunga huwa tunatoa siku 14 mhusika akalipe na baada ya hapo sasa tunasubiri maelekezo kutoka kwa TRA.”

Juhudi za kumpata Manji na wasaidizi wake zilishindikana.

Chanzo: Mwananchi