Vincent Kigosi ‘Ray’.
MSANII wa Bongo Movie’s, Vincent Kigosi ‘Ray’ amewaambia mashabiki wenzake wa Yanga kuwa, wasihofi mabao ya Emmanuel Okwi wa Simba, kwani huwa anazifunga timu ndogo tu.
Yanga leo Jumamosi inacheza na Simba kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam mechi ya Ligi Kuu Bara raundi ya nane.
Mpaka sasa Okwi ndiye kinara wa mabao akiwa nayo nane.
Ray alisema: “Yanga ipo vizuri kila idara hivyo na ninaamini haitatuangusha kwenye mchezo huu ingawa wapinzani wanapiga kelele za Okwi, watambue kuwa huyo haiwezi Yanga.
“Okwi anaonekana katika mechi ndogo lakini katika mechi kubwa anafunikwa hivyo wasitegemee jipya kutoka kwake.”