F Taarifa ya watoto 9 kufariki kutokana na kukatika kwa umeme yakanushwa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Taarifa ya watoto 9 kufariki kutokana na kukatika kwa umeme yakanushwa

Mganga Mkuu Mkoa wa Arusha Dkt. Wonanji Timoth amekanusha taarifa za kufariki kwa watoto 9 waliokuwa kwenye Incubator kutokana na katizo la umeme hapo jana hospitali ya Mt. Meru, na kusema kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote.

Dkt. Timoth amesema kwamba watoto waliofariki walikuwa wanne na sio 9 kama inavyoelezwa kwenye taarifa iliyosambaa mitandaoni, na wamefariki kwa matatizo mengine lakini sio kukatika kwa umeme.

Dkt. Timoth ameendelea kwa kueleza kwamba moja ya sababu iliyofanya watoto hao kufariki ni mama kuchelewa kufika hospitali kujifungua kwa kuwa alijifungulia nyumbani, pamoja na hatari kubwa wanazopata watoto njiti.