Fuvu la kichwa lililokutwa kwenye bwawa la maji.
Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Simon Haule amedai kuwa jana watu walipoona viungo hivyo vya binadamu ilibidi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi na wao walifika na kukuta viungo hivyo.
"Fuvu la kichwa limepatikana hapo bwawani, taya ya binadamu, mbavu za binadamu kumi na nne, baada ya kupatikana kwa taarifa hizo jeshi la polisi lilichukua hatua za haraka kufika eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi wa awali tukishirikiana na daktari mtaalam wa viungo vya binadamu katika tukio hilo tulikuta viungo hivyo ikiwa pamoja na mfupa mmoja wa sehemu ya paja, mifupa ya mikono na mifupa ya sehemu ya bega ya binadamu" alisema Simon Haule
Aidha Kamanda Haule amesema kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ikiwa pamoja na kufungasha mifupa yote na kupeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kufanya vipimo kubaini vinasaba na jinsia ya mtu ambaye amefariki.