F Wananchi waendelea kupiga kura Kenya | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wananchi waendelea kupiga kura Kenya

Wananchi nchini Kenya leo wanapiga kura kwenye uchaguzi wa marudio wa rais, baada ya matokeo yake kufutwa na mahakama Septemba 1, mwaka huu.

Uchaguzi huo ambao umegubikwa na vurugu mbali mbali kwa baadhi ya maeneo, unaendelea huku kukiwa na mvua kubwa na kuleta kikwazo kwa baadhi ya maeneo kwenda kupiga kura.

Katika baadhi ya maeneo ikiwemo Kibera ambayo ni kambi kubwa ya NASA, yamekuwa na vurugu kwa kujaribu kukwamisha zoezi hilo la upigaji kura, kwa kufunga njia za kwenda kwenye vituo vya kupigia kura, kitendo kilichopelekea polisi kuingilia kati na kuzifungua njia hizo, pamoja na kupiga mabomu ya machozi ili kutuliza ghasia.

Maeneo mengine yameonekana kufurika watu na kuendelea na zoezi la kupiga kura, licha ya changamoto hiyo kubwa ya mvua, ambayo pia imepelekea kukwama kwa baadhi ya magari yaliyokuwa yakisafirisha vifaa vya kupigia kura.

Katika eneo la Garisa askari polisi mmoja amefariki na wengine watatu kujeruhiwa, baada ya gari walilokuwa wakitumia kusafirisha makaratasi ya kupiia kura kupata ajali.