F Majaliwa akiruhusu chuo kikuu huria kutoa kozi ya Foundation | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Majaliwa akiruhusu chuo kikuu huria kutoa kozi ya Foundation


Chuo Kikuu Huria pekee kimepewa ruhusa ya kuendelea kutoa kozi ya Foundation iliyokuwa imesitishwa na serikali kwa wanafunzi ambao wamekosa vigezo vya kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu baada ya mtaala wake kuboreshwa na kupitishwa na Wizara ya Elimu.

Ruhusa hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa leo akiwa mkoani Singida yanapofanyika Mahafali ya chuo hicho.

Ikumbukwe kuwa Mwaka 2016 Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella Manyanya alitoa katazo hilo na kusema utaratibu wa kozi ya Foundation umefanywa na  vyuo  vyenyewe hivyo serikali haiwezi kuukubali mfumo wa  elimu hiyo na kwamba kama mtu anasoma kozi ya Foundation apewe cheti na kama atahitaji  kujiendeleza asafishe cheti au asome mfumo ambao utamfikisha katika shahada.

Mbali na hayo katika Mahafali hayo ambayo Waziri Mkuu ndiye Mgeni rasmi atamtunuuku mkewe Bi Mery Shahada ya Uzamiri ya Elimu. 


"Wakati najiandaa kuja kwenye sherehe mwenzangu naye kumbe anajiandaa,  nashukuru amemaliza sasa mambo nahisi yataenda vizuri maana wakati mambo ya masomo yalipokuwa busy hata tulikuwa hatuonani...Leo pia naona familia yangu nayo itakuwa inasherehekea" Majaliwa
Majaliwa
Pamoja na hayo Waziri Mkuu amejipigia debe sherehe ya mahafali yajayo yakafanyike mkoani Lindi pia kwani wamejiandaa vyema