F Ufaransa: Chama tawala chachagua kiongozi mpya | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Ufaransa: Chama tawala chachagua kiongozi mpya

Chama tawala cha rais wa sasa Emmanuel Macron kimemchagua kiongozi wake mpya.

Kwa mujibu wa habari,ni miezi 19 toka chama hicho cha LREM(La Republique En Marche) kiundwe.

Msemaji wa serikali Christophe Castaner ndie amechaguliwa kama kiongozi mpya wa chama hicho.

Chama hicho kimefanya mkutano wake wa kwanza mashariki mwa mji wa Lyon.

Mgombea pekee wa nafasi hio, Castaner, 51, amechaguliwa kama kiongozi wa chama hicho na viongozi waliochaguliwa, mawaziri, watendaji wa chama na wanachama 200 wa chama.

Christophe Castaner hakuchaguliwa moja kwa moja na wanachama  380,000 wa LREM.

Atatumikia nafasi yake kwa muda wa miaka mitatu.