F Chanzo cha Fangasi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Chanzo cha Fangasi

Fangasi ni nini
Watu wengi hawajisikii vizuri unapokuja wakati wa kuzungumza juu ya fangasi kutokana na namna ugonjwa wenyewe unavyochukuliwa na jamii. Hii inatokea sababu mara nyingi ugonjwa huu hutokea sehemu ambazo ni aibu kuzizungumzia au kuzionyesha hadharani.

Fangasi mara nyingi inawapata zaidi watu wanaoishi kwenye maeneno ya joto kuliko wale wanaoishi maeneno ya baridi kutokana na vimelea vya ugonjwa wenyewe kushamiri zaidi sehemu za joto.

Pamoja na hayo yote fangasi ni ugonjwa wa kawaida ambao unaweza kumpata mtu yeyote, mimi mwenyewe nimewahi kupatwa na fangasi sehemu za siri na zilinisumbuwa sana. Takwimu zinadai katika kila watu watano mmoja kati yao anapatwa na maradhi haya katika safari yake ya kuishi kwa hapa Tanzania.

Hapo awali fangasi walikuwa wanahesabika kama ni aina mojawapo ya mimea lakini baadaye sayansi imekuja kugunduwa kuwa fangasi hawana sifa za kuwekwa katika kundi la mimea.

Kuna fangasi wa aina nyingi lakini tunaweza kuwaweka kwenye makundi makubwa mawili ambao ni fangasi wanaoleta madhara ya kwenye ngozi na fangasi ambao maisha yao yote wanaishi kwenye ngozi wakiitegemea hiyo tu ili waweze kuishi.

Vimelea hivi vya fangasi vinavyokaa kwenye ngozi vimegawanyika tena katika sehemu kuu mbili, kundi la kwanza ni wale wanaojulikana kwa kitaalamu kama dermatophytes au dematofaiti kwa kiswahili na hamira au yeast kwa kiingereza

Kwahiyo kama ulikuwa hufahamu, basi leo fahamu kuwa hamira yaani hamira ile inayotumika wakati wa kupika maandazi na hata mikate ni fangasi.  Fangasi huishi kwenye ngozi kwakuwa hutegemea protini inayopatikana kwenye ngozi ambayo huitwa keratini (keratin).

Keratini ni protini ya muhimu sana katika ngozi na inatengeneza asilimia kubwa ya ngozi, kucha na nywele ambako kama umeshagundua mpaka sasa ni sehemu ambazo fangasi hupenda sana kushambulia kuliko sehemu nyingine za mwili.

Kwahiyo utagundua kuwa sababu kubwa ya waTanzania wengi kuugua fangasi ni hii protini ya kwenye ngozi ijulikanayo kama keratini, joto na uwepo wa hali ya unyevu unyevu katika maeneno mengi hasa ukanda wa pwani.

Kwa hali ya kawaida, fangasi wa aina hii huwa hawana madhara makubwa, wao huweka makazi yao tu kwenye ngozi bila kusababisha hali yoyote ya madhara kwenye ngozi. Madhara ya vimelea hivi huonekana baada ya idadi kubwa ya vimelea hivi kuongezeka kwenye eneo dogo moja la ngozi.

Fangasi ni ugonjwa unaoambukiza kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine ikiwa watu hao watashirikiana mavazi na vifaa vingine vya usafi wa mwili.

Madhara ya Fangasi katika ngozi
Vimelea vya fangasi huathiri ngozi moja kwa moja kwa kuvamia na kutafuna keratini ambayo ni protini muhimu ya ngozi ikiwa inatengeneza sehemu kubwa ya ngozi, kucha na nywele.

Aina za maradhi ya ngozi yanayosababishwa na fangasi

Kuna aina nyingi za maradhi ya ngozi ambayo chanzo chake huwa ni fangasi na hayo yote yameganwanywa katika sehemu kuu mbili: