F Diwani wa Chadema afunguka kuhama chama kwa masharti | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Diwani wa Chadema afunguka kuhama chama kwa masharti


Diwani wa (CHADEMA), Kata ya Sombetini, Ally Bananga amesema yupo tayari kurudi  (CCM) ikiwa viongozi wa chama hicho ambao wanataka kumnunua ikiwa watamuonyesha watu waliowatuma kumuua Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.

Ally Banaga amedai kuwa yeye yupo tayari kurudi CCM kama viongozi hao watatimiza jambo hilo na kusema hiyo ndiyo itakuwa gharama yake kurudi CCM na siyo fedha au mali kama ambavyo wengine wanadaiwa kupewa.

"Ma CCM wanaotaka kuninunua, leo nataja gharama za kurudi CCM. Nionyesheni mliowatuma kumuuwa Mawazo, nitajiunga nanyi siku hiyo hiyo" alindika Ally Banaga

Aidha Banaga ameonyesha masikitiko yake makubwa kwa watu ambao wanakisaliti chama hicho na kusema kuwa wamesahau kuna watu kama kina Mawazo ambao wamekufa wakikipigania chama hicho.

"Nilishika jeneza lako nikikuangalia mwamba umelala. Ndipo nilipoamini kuwa sio stori, mwanaume wa kweli uliyefia vitani ukikitetea chama ambacho kuna Mambwa Koko yanakisaliti, yanakichezea yanakinajisi bila kuhisi maumivu yako ulipotoka roho kukipigania. Nilikuita kwangu Dar es Salaam tupumzike baada ya uchaguzi mkuu ambao CCM walikupora kwa nguvu ushindi wako, kaka ukakataa kwa neno moja " Nikiondoka Makanda watakufa moyo, ngoja niwape tafu, Tukutane Dodoma.....dah! Tukakutania Mwanza kwenye jeneza" alisema Banaga

Novemba 14, 2015 aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Busanda kupitia CHADEMA na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Geita aliuawa kwa kupigwa mapanga na watu wasiojulikana na kupelekea kifo chake.