F Msigwa awapongeza Kakobe, Gwajima | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Msigwa awapongeza Kakobe, Gwajima


Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Peter Msigwa amefunguka na kuwapongeza baadhi ya viongozi wa dini akiwepo Askofu Zakaria Kakobe, Askofu Josephat Gwajima, Askofu Benson Bagonza kwa kile walichofanya kukemea baadhi ya matendo ya serikali

Mchungaji Msigwa ameweka wazi kuwa hicho kilikuwa kilio chake kikubwa kwa viongozi wa dini kwani Tanzania inapaswa kujengwa na watu wote na si wanasiasa tu

"Nawapongeza sana baadhi ya viongozi wa dini kama vile Askofu Kakobe, Askofu Gwajima, Askofu Bagonza na Shayo ambao kwa namna moja kimekuwa kilio changu kikubwa pamoja na wananchi wengine kuona viongozi wa dini wanakuwa kimya wakati mambo hayaendi vizuri, Kwa kifupi niwapongeze sana kwa sababu nchi hii inajengwa na sisi sote na mali yetu sote" alisema Msigwa

Aidha Mchungaji Msigwa aliendelea kusema kuwa yeye amesikitiswa na baadhi ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wanataka kulifanya Taifa la Tanzania lisiwe la watu wa kufikiri

"Hoja alizotoa Askofu Kakobe zinafafanua vizuri na kuwafanya watu wafikiri na kujibu kwa hoja lakini watu wameanza kumshambulia kwa kejeli na maneno ambayo si ya kiugwana, hoja siku zote hujengwa kwa hoja hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria, Kakobe alimuomba Mhe. Magufuli akatubu kwamba anaiendesha nchi kama vile nchi ya chama kimoja" Alisisitiza Msigwa