Baada ya tetesi za muda kampuni ya Apple imetangaza rasmi kuinunua App maarufu ya kutambua muziki ya Shazam.
Katika taarifa iliyotolewa na pande zote mbili kulionesha mafanikio yaliyofikiwa kwa makubaliano yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 400 sawa na pesa ya Tanzania yenye thamani ya 897,580,000,000.
Apple wamesema wanafuraha kwa shazam kujiunga nao na wana mipango mizuri juu ya uboreshaji wa App ya Shazam. Kwa upande wa Shazam wamesema wamefanya makubaliano kuwa sehemu ya timu ya Apple.
Shazam ni moja ya programu zinazopendwa na kupakuliwa sana na mamilioni ya wengi duniani ambapo kazi yake kubwa ni kutambua muziki wowote ambao unautafuta.
Mfano kuna muziki unausikia na ungependa kujua umeimbwa na nani unachofanya ni kufungua App ya Shazam na kusikilizisha muziki huo na punde itautambua muziki huo kwa jina lake na ni nani aliyeuimba.
Kununuliwa kwa Shazam kunaweza kuwa pigo kwa watumiaji wa simu za mfumo wa Android kwani kuna uwezekano mkubwa App hiyo kuondolewa katika Play store na kubaki kwenye duka la AppStore pekee.