Mwanamuziki Lady Jaydee amefunguka ni kwanini hatoi ngoma kila mara.
Muimbaji huyo amesema si utaratibu ambao ameuzoea katika muziki wake na wale wanaofanya hivyo si vibaya pengine kuna faida wanayoipata huko.
“Mimi huwa sitoi ngoma hivyo, huwa sitoi ngoma kila siku, kwa hiyo kwa wanatoa ngoma kila siku wanazo sababu zao pia labda wenyewe wanaweza wakaelezea ni kwanini pengine inaweza ikawa na manufaa kwao ndio maana wanafanya vile,” amesema.
Lady Jaydee ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Baby’, wimbo huo umepishana takribani miezi mitatu na I Miss You.