F Mama afunguka kuhusu Nabii Tito na Kanumba | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mama afunguka kuhusu Nabii Tito na Kanumba


BAADA ya picha kusambaa za aliyekuwa staa wa sinema za Kibongo, Steven Kanumba akiwa na Nabii Tito ambaye kwa sasa yupo mbaroni kutokana na kuonekana akikashifu dini, mama mzazi wa staa huyo, Flora Mtegoa na mdogo wake, Seth Bosco wamemfungukia jamaa huyo jinsi alivyokuwa akiwashawishi kujiunga naye.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mama Kanumba alisema kuwa, alisikia Nabii Tito alikuwa akimshawishi Kanumba aingie kwenye dini yake, lakini hakukubaliana naye kwa kuwa alikuwa ana imani na msimamo mkali wa kidini hivyo ikawa ni vigumu kumkubalia.

Kwa upande wake, Seth alisema kuwa, Nabii Tito alifika ofisini kwao, Sinza-Mori, Dar, kipindi hicho wakiwa na Kanumba akawahubiria na kuwashawishi wajiunge naye, lakini walikataa na ndiyo siku waliyopiga naye picha.