F Marufuku michango ya Elimu yazua mjadala kwa Viongozi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Marufuku michango ya Elimu yazua mjadala kwa Viongozi


UAMUZI wa Rais John Magufuli kupiga marufuku michango ya elimu katika shule za msingi na sekondari, umezua mjadala katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Kahama mkoani Shinyanga.

Madiwani hao walitaka kupata ufafanuzi kutoka uongozi wa halmashauri kutokana na wananchi kukataa kutoa michango ya elimu baada ya serikali kusisitiza kuwa imefutwa kutokana na mpango wa elimu bure,

Kutokana na hali hiyo,  baadhi ya madiwani walimtaka  Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Anderson Msumba, kutoa maelezo kuhusiana michango hiyo ambayo ilipigwa marufuku na Rais Magufuli hivi karibuni.

Katika kikao cha madiwani kilichofanyika mwishoni mwa wiki, Diwani wa Nyihogo, Shadrack Mgwabi, alimtaka mkurugenzi huyo atoe ufafanuzi juu ya michango iliyofutwa kwenye shule za msingi na sekondari.

Mgwabi alisema hivi sasa wananchi wengi wamegoma kabisa kuchangia elimu, hatua ambayo ni  changamoto kubwa kwa sasa kutokana na nguvu za wananchi kupitia michango  ndiyo zilikuwa zikisaidia maendeleo shuleni.