F Owenya, Pareso wamchongea Dk Mollel kwa wananchi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Owenya, Pareso wamchongea Dk Mollel kwa wananchi

Wabunge wa viti maalumu (Chadema), Lucy Owenya na Cecilia Pareso wamewataka wananchi wa Jimbo la Siha kutomchagua mgombea wa CCM, Dk Godwin Mollel.

Awali Mollel alikuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema lakini Desemba 14 mwaka jana alijiunga CCM na anagombea tena nafasi hiyo kupitia chama tawala.

Wabunge hao walitoa ombi hilo leo Januari 26, mwaka 2018 katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika kijiji cha Ngarenairobi na kuwataka wananchi wamchague mgombea wa Chadema, Elvis Mosi.

Wamesema Dk Molell aliwaomba wananchi hao wamchague kuwa mbunge katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kwamba walimpa heshima hiyo wakati akiwa Chadema, lakini alijiuzulu na kutimkia chama kingine.

Uzinduzi wa kampeni hizo unaongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe