F Ruvu Shooting yaamka na kuichapa Mbao FC 2-0 | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Ruvu Shooting yaamka na kuichapa Mbao FC 2-0

Klabu ya ligi kuu soka Tanzania Bara Ruvu Shooting ya mkoani Pwani imepanda kwenye msimamo wa ligi baada ya leo kuibuka na ushindi katika mchezo wake wa raundi ya 15 dhidi ya Mbao FC.

Mchezo huo ambao umepigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Mlandizi Pwani Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 hivyo kutoka mkiani mwa msimamo na kupanda kutoka nafasi ya 16 hadi ya 11 baada ya kufikisha alama 14.

Mabao yote ya Ruvu Shooting leo yamefungwa na Khamis Mcha katika dakika za 26 na 44 na kupeleka kipigo cha pili mfululizo kwa klabu ya Mbao FC ya jijini Mwanza.

Mechi iliyopita Mbao FC ilipokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Stand United, kwenye mechi iliyopigwa uwanja wa CCM Kirumba. Timu hiyo imebaki katika nafasi ya nane ikiwa na alama 15.