F Eto’o kavunja mkataba na kujiunga na timu hii | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Eto’o kavunja mkataba na kujiunga na timu hii

Aliyekuwa anaichezea club ya Antalyaspor ya Uturuki Samuel Eto’o, ametangazwa kuvunja mkataba na kujiunga na club ya Konyaspor ya Ligi Kuu Uturuki.

Eto’o ambaye alijiunga na Antalyaspor 2015 na amedumu nayo kwa miaka miwili lakini ameamua kujiunga na Konyaspor baada ya kuvunja mkataba na Antalyaspor kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Samuel Eto’o amewahi kuvichezea vilabu mbalimbali kwa mafanikio ikiwemo FC Barcelona aliyoichezea na kushinda Champions League mara mbili na LaLiga mara tatu kuanzia mwaka 2004-2009.

Baadae Eto’o alijiunga na Inter Milan iliyokuwa chini ya Jose Mourinho  na kufanikiwa kushinda taji la Champions League, Serie A na Coppa Italia na baadae akaenda Anzhi Makhachkala ya Urusi halafu Chelsea, Everton na akacheza pia kwa muda mfupi Sampdoria ya Italia kabla ya kwenda Uturuki.