F Hii ndio rekodi aloiweka Messi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Hii ndio rekodi aloiweka Messi


NYOTA wa Klabu ya Barcelona na Timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi, amevunja rekodi ya kutofunga goli lolote dhidi ya Chelsea ya Uingereza pindi timu hizo zinapokutana.

Imemchukua mchezaji kutumia dakika 730 na mechi 9 kufunga bao lake la kwanza katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya (UEFA), ikiwa ni dakika ya 75 ya mchezo usiku wa kuamkia leo.

Messi ambaye amekuwa yuko katika kikosi kimoja na Andres Iniesta tangu aanze kuichezea Barcelona, alikuwa hajawahi kuzitikisa nyavu za Chelsea hata mara moja.

Iniesta ndiye alimsaidia Messi kufunga bao hilo kwa pasi safi ikitokea upande wa kushoto mwa uwanja wa Stamford Bridge na kuizamisha nyavuni fasta.

Bao lake la kusawazisha limekuwa muhimu kwa Barcelona ambayo imekuwa na faida ya goli moja la ugenini, kabla timu hizo hazijakutana tena katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Camp Nou, Jumatano ya Machi 14, 2018.