Baada ya kupita takribani kwa masaa 35 tangu Zari The Bosslady kutangaza kuachana na Diamond, mrembo huyo ameibuka na ujumbe mpya ambao unaonekana kama ametupa jiwe gizani.
Kupitia mtandao wa Instagram leo (Ijumaa), mrembo huyo amepost picha mbili zenye ujumbe tofauti. Katiaka picha ya kwanza ambayo ameiweka kwenye mtandao huo, Zari ameandika, “Consistency is key #Mompreuer.”
Wakati huo huo kwenye picha nyingine malkia huyo ameandika, “Me when people ask what I do…. whatever it takes👌.”