Serikali ya Kenya imeingia mkataba wa dola $57.2 millioni ambazo ni Ksh5.8 billioni (sawa na TZS 128.7 bilioni) na Kampuni ya Doppelmayr Group ya Austria kwa ajili ya ujenzi wa magari yanayotembea kwenye nyaya (cable cars).
Kampuni ya Doppelmayr inatarajiwa kuanza rasmi ujenzi wa mradi huo wa kiteknolojia Mwezi Mei mwaka huu na kukamilisha mwaka 2020.
Wadhamini wa mradi huo ambao ni Trapos Limited na Kenya Ferry Services (KFS) zilisaini mkataba huo wa mabilioni ya pesa tangu Desemba mwaka jana ambapo mchakato wa ujenzi wa mradi huo sasa upo njiani.
Mkurugenzi Mtendaji wa KFS, Bakari Gowa alitoa taarifa juzi Alhamisi kuwa, kwa sasa wataalam wanamalizia upimaji na uwekaji alama wa maeneo ya barabara ambapo mradi huo utaweza kupita kwa urahisi.