F Rais Magufuli ashiriki Misa ya majivu | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Rais Magufuli ashiriki Misa ya majivu


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki na wakristo wengine katika ibada ya Jumatano ya majivu inaoashiria kuanza kwa mfungo mtukufu wa kwaresma.

Magufuli akiwa na mkewe, Mama Janeth Magufuli wameungana na waumini hao katika ibada iliyoongozwa na Muadhama Askofu Mkuu, Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Dar, leo Februari 14, 2018.