Na James Timber, Mwanza
Chama Cha Wauguzi Nchini (TANNA) kimelaani tukio la shambulio Muuguzi lililotokea tarehe 18 mwezi huu katika Hosptali ya Bugando jijini Mwanza.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema hiii leo Makamu wa Rais wa Chama cha Wauuguzi nchini Dk.Ibrahim Mgoo, amesema kuwa kabla ya shambulio hilo muuguzi alitimiza wajibu wake wa kazi , alishambuliwa na watu wanaojulikana wiokuwa na kusudi la kutoa uhai katika chumba cha uangalizi maalumu (HDU), Hosptalini hapo, ambapo ni kinyume na taratibu za hosptalini hapo.
"Kabla ya mauti kumfika mgonjwa huyo ndugu zake walilazimisha wabaki katika chumba hicho jambo ambalo, halikukubaliwa na muuguzi huyo kesho yake walipotarifiwa ndugu yao amefariki, ndipo walipoamua kufanya kitendo cha cha unyama na udhalilishaj kwa kumshambulia na kumjeruhi muuguzi alipokuwa anatoa huduma kwa wagonjwa wengine", alisema.
Makamu Mgoo, ameviomba vyombo vinavyohusika kuchukua hatua stahiki, kwa wahusika mapema ili kutoathiri utendaji wa wauguzi nchini, ikiwa ni pamoja na kuboresha ulinzi wa wauguzi na watumishi wengine mahala pa kazi ili kutoleta madhara makubwa katika kazi.
Aidha, ametoa shukrani kwa hatua zilizochukuliwa na uongozi wa Hosptali ya Bugando ukishirikiana na chama cha wauguzi, kuhakikisha Muuguzi huyo anatendewa haki katika vyombo vinavyohusika.