Tanzia: Msanii Radio kutoka Uganda afariki Dunia

Muimbaji kutokea kwenye kundi la Good Lyfe Moses Sekibooga ambaye wengi wanamfahamu Radio kutokea Uganda imeripotiwa amefariki dunia asubuhi ya leo February 1,2018 baada ya kukaa ICU kwa siku kadhaa zilizopita, hii ni baada kuripotiwa kupata ajali ya gari  January 23,2018.

Muimbaji Radio ameacha pengo kubwa katika kundi la Good Lyfe ambalo liliundwa na yeye mwenyewe pamoja na Weasel ambaye ni mdogo wa muimbaji na legend wa muziki nchini Uganda Joseph Mayanja ambao wengi tunamfahamu kama Jose Chameleon.

Taarifa za kifo cha Radio zinakuja ikiwa ni siku moja imepita toka Rais wa Uganda Yoweri Museveni kuripotiwa kutoa milioni 30 kama mchango kwa ajili ya kuokoa maisha ya staa huyo kwa kugharamia matibabu.

Radio na Weasel wamefanya nyimbo nyingi ambazo zimewahi pia kupata Air time katika TV  na Radio Stations za Tanzania, Don’t Cry ft Wizkid, Zuena na wimbo wa Where You Are waliokuwa wameshirikishwa na Blu 3 na huu uliwafanya wajulikane zaidi Tanzania kutokana na wimbo huo kufanya vizuri.