F TTCL yabadilishwa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

TTCL yabadilishwa

picha ya mtandao

Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania leo Februari 1, 2018 imefanya mabadiliko na kuibadili kampuni ya simu ya TTCL kuwa shirika la Umma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametangaza maamuz hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa mabadiliko hayo hayawezi kuathiri wateja wa TTCL 

"Sasa tunatoka kwenye TTCL kampuni na kuwa shirika la Umma tunaamini saizi mtajipanga zaidi kwenye mambo ya usalama na uimarishaji mambo ya uchumi. Pia napenda kuwajulisha Watanzania kuwa mabadiliko haya hayatawaathiri kwa namna ya utoaji wa huduma mbalimbali ambazo zilikuwa zikitolewa na kampuni ya simu ya TTCL, huduma zote zilizokuwa zikitolewa kuanzia kwenye simu za mkononi, data, enternet, TTCL Pesa zote zitaendelea sasa kwa kiwango kikubwa zaidi" alisema Mbarawa 

Mbali na hilo Mbarawa amewataka TTCL sasa kufanya jitihada za kwenda kukusanya madeni yake kwa wananchi mbalimbali ambao wanatumia huduma zao na kusema kuwa Serikali inatambua ina deni kwa TTCL na kuwa wao watalipa na wako tayari kulipa ila wanapaswa kuanza kwenda kudai fedha zao kwa wananchi mbalimbali na makampuni ambayo pia yanadaiwa na TTCL.