Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Agustino Senga
Wiki mbili zilizopita Mnyeti aliagiza vigogo hao wa madini kukamatwa na kushikiliwa kwa saa 48 kwenye kituo cha polisi Mirerani wakidaiwa kufadhili uchimbaji huo haramu.
Akizungumza leo Februari 23, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Agustino Senga amethibitisha vigogo hao wa madini kusafirishwa licha ya kuwa walipatiwa dhamana, polisi wakawashikilia na kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Amesema waliwashikilia wachimbaji hao baada ya kamati iliyoundwa na mkuu wa mkoa huo kupata taarifa kuwa vigogo hao wanashiriki kuwadhamini vijana wanaoingia kwa wizi kwenye migodi ya kampuni ya TanzaniteOne yenye ubia na Serikali kwa asilimia 50 kwa 50 na Shirika la Madini la Taifa (Stamico).
Amesema kuna kamati maalum iliundwa na mkuu wa mkoa huo kwa ajili ya kuchunguza suala hilo hivyo baada ya uchunguzi wa awali, ikabidi vigogo hao wakamatwe.