Idara ya afya ya Mashariki mwa Cape own nchini South Africa ilitoa onyo baada ya watu zaidi ya 50 ambao walikula nyama ya ng’ombe waliokufa kupelekwa hospitali mbalimbali Alhamisi katika jimbo hilo.
Wagonjwa hao walikuwa na dalili ikiwa ni pamoja na kuhara, kutapika, maumivu ya kichwa na ya tumbo. Wao walielezea kwamba walikuwa wamekula nyama ya ng’ombe aliyekufa baada ya kuumwa na nyoka.
Sizwe Kupelo ammaye ni msemaji wa jimbo hilo ,alisema kwamba wagonjwa walifikishwa hospitali ya Dr Malizo Mpehle huko Tsolo.
Watoto 16 pamoja na wazee 4 baadaye walihamishiwa hospitali ya Nelson Mandela na Hospitali ya Mkoa wa Mthatha ya nchini South Africa ili kupata matibabu kutoka kwa wataalamu.