Zimbabwe: Kamisheni ya Amani na Maridhiano yaanza kusikiliza tuhuma za ukatili na mauaji

Kamisheni ya amani na maridhiano nchini Zimbabwe,(NPRC),leo imeanza kusiliza tuhuma za waathrika wa vitendo vya kikatli na mauaji vilivyotekelezwa nchini humo miaka 30 iliyopita wakati wa utawala wa Robert Mugabe.

Katika shauri hilo la wazi,imedaiwa kuwa rais huyo wa zamani wa Zimbabwe,aliamuru kuuawa kwa watu katika jimbo la Matebele,alioamini kuwa walikuwa wanajaribu kumuondoa madarakani.

Hata hivyo wengi wanahisi kuwa shauri hilo linalosikilizwa na Kamisheni hiyo,ni kupoteza muda kwakuwa imewekwa na serikali.

Imeelezwa kuwa wakati wa mauaji hayo,yaliyogharimu maelfu ya wananchi wa eneo hilo,Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa,alikuwa waziri wa usalama wa ndani wa nchi