F Arnold Schwarzenegger afanyiwa upasuaji wa moyo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Arnold Schwarzenegger afanyiwa upasuaji wa moyo

Mwigizaji maarfu wa Hollywood Arnold Schwarzenegger amefanyiwa upasuaji wa moyo.

Arnold Schwarzenegger ambae amecheza katika filamu takriban 50 na alikuwa gavana wa zamani wa California amefanyiwa upasuaji wa moyo ambao umemalizika salama usalimini.

Meneja wa nyota huyo amesema kuwa mnamo mwaka 1997 Arnold Schwarzenegger aliwekewa "pulmonary valve",na upasuaji huu umefanywa ili kumuwekea "pulmonary valve" mpya.

Kama kawaida katika filamu zake Schwarzenegger hutumia sana neno la "I'll be back"na baada ya upasuaji amerekodiwa akisema, "I am back".

Arnold Schwarzenegger, ambaye alianza kujenga mwili wakati wa umri wa miaka 15.

Alishinda tuzo ya Mr.Universe akiwa na umri wa miaka 20.